Mwanafunzi mmoja wa chuo cha mafunzo Wilaya ya Wete, Pemba aliyejulikana kwa jina la, Hemed Suleima Seif (40) amefariki baada ya kupigwa na shoti ya umeme wakati akijaribu kufanya matengenezo.
Inaelezwa kuwa kabla ya kukutwa na umauti, mwanafunzi huyo alikuwa akifundishwa ujuzi wa matengenezo ya Umeme kwa vitendo na mwalimu wake.
Akithibisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa polisi mkoa wa Kaskazini Pemba, Sheikhan Mohammed Sheikhan amesema tukio hilo limetokea saa 1:45 za asubuhi, wakati marehemu akiwa chini ya mwalimu wa fani hiyo wakijaribu kurekebisha kasoro katika moja ya nguzo ya jengo.
“Ni kweli tumepokea taarifa kutoka kwa wenzetu wa chuo cha mafunzo kuwa kuna mwanafunzi anaetambuliwa kwa jina la Hemed Suleiman, amefariki baada ya kupigwa na shoti ya umeme,” amesema.
“Tayari maiti imekabidhiwa jamaa zake kwa mazishi na jeshi la polisi inatoa pole kwa wafiwa,” ameongeza.
Kamanda Sheikhan pia amesema uchunguzi wa awali uliofanywa na madaktari wa hospitali ya Wete umebainisha kuwa marehemu aliathirika mwili mzima. Amewaomba wananchi kuwa waangalifu wakati wanapokua katika harakati zao hasa za kushughlikia masuala ya umeme.
Mwanafunzi wa Chuo Afariki Juu ya Nguzo ya Umeme Akifanya Matengenezo
0
December 21, 2018
Tags