Mwanamke Mmoja Nchini Argentina Aachiwa Huru Baada ya Kutekwa kwa Miaka 30

Mwanamke Mmoja Nchini Argentina Aachiwa Huru Baada ya Kutekwa kwa Miaka 30
Mwanamke mmoja raia wa Argentina ameokolewa na polisi baada ya kushikiliwa mateka kwa zaidi ya miaka 30.

Operesheni ya kumnasua mwanamke huyo ilifanyika kwa ushirikiano wa polisi wa nchi za Argentina na Bolivia.

Mahala ambapo alikuwa akishikiliwa mwanamke huyo ambaye sasa ana umri wa miaka 45 lilikuwa halifahamiki toka miaka ya 80.

Hata hivyo, mapema mwaka huu, polisi walipata taarifa kuwa alikuwa akishikiliwa katika eneo la Bermejo, kusini mwa Bolivia.

Baada ya uchunguzi, polisi walifanikiwa kuitambua nyumba aliyokuwemo na kufanikiwa kumuokoa akiwa na mtoto wake mwenye umri wa miaka tisa.

Majina ya mwanamke huyo na mtoto wake ambao waliokolewa mwanzoni mwa mwezi Disemba hayajatajwa na vyombo vya usalama.

Katika taarifa iliyotolewa Disemba 25, polisi nchini Argentina wanasema walau mwanamke huyo amefanikiwa kurejeshwa na kuungana na familia yake katika mji wa Mar del Plata.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad