Mwenyekiti wa Matawi ya Yanga huko Zanzibar, Ally Makolo amewalaani baadhi ya wanachama wa timu hiyo wanaokataa klabu uao kufanya uchaguzi Januari 13 mwakani.
Makolo amesema kitendo hicho si cha busara na ni kibaya kwani watakuwa wanaenda kinyume na taratibu za serikali kwa vile imepanga ratiba hiyo na ni lazima itekelezwe.
Kwa mujibu wa Radio One, Mwenyekiti huyo amewataka wanacha wote kuitikia wito wa kufanya uchaguzi huo kwani ni kwa mujibu wa katiba ya Yanga yenyewe kuwa klabu haiwezi kuendeshwa bila kuwa na kiongozi.
Aidha, amewalaani pia wale waliotishia kwenda mahakamani kwa ajili ya kupinga uchaguzi akieleza ni kitendo ambacho si cha kiungwana hata kidogo.
Mwisho kabisa amehimiza na kuwataka wanachama wote wa Yanga kujipanga kuelekea uchaguzi huo ambao utampata pia Mwenyekiti ambaye atadumu mpaka mwaka 2020.