Nahisi Rafiki Yangu Anataka Nimsaidie Kumtia Mimba Mke Wake
0
December 14, 2018
Kuna jamaa yangu yupo kwenye ndoa kwa miaka saba na hajafanikiwa kupata mtoto..hivi karibuni analikuwa ananipigisha stori fulani hivi ambazo nilikuwa sizielewielewi kuhusu wanaume wengine kutumika kuwapa mimba wake za watu
Juzi amekuja kutoka Morogoro amekuja nyumbani kwangu Dar anasisitiza anataka nimsaidie kutafuta dawa ili mkewe apate ujauzito eti wamekubaliana na mkewe wanishirikishe mimi kwa sababu ni msiri na mstaarabu.
Ili mke wake apate ujauzito kumbuka mimi siyo daktari. Alivyoona nakuwa mkali akaniambia atanipigia simu akifika Morogoro ili tujadiliane vizuri.
Ameondoka leo asubuhi kimsingi mimi sijaoa na sijaona sababu ya kufanya ujinga huo. Wanajukwaa mimi msimamo wangu ni hapana.
Ushauri tafadhali
Tags