Oparesheni kubwa ya uokoaji inaendelea nchini Japan kuwatafuta wanajeshi watatu wa Marekani bbada ya ndege mbili zilizokuwa na wanajeshi saba kugongana na kuanguka baharini.
Wanajeshi wawili waliokolewa. Mmoja wao yuko hali nzuri kwa mujibu wa wa wizara ya ulinzi nchini Japan. Hali ya mwanajeshi mwingine haikujilikana mara moja.
Ndege hizo zilikuwa za KC-130 na F/A-18 kutoka kambi ya Iwakuni karibu na Hiroshima.
Vyombo vya habari vya Marekani vinasema ndege hizo zilianguka wakati wa kuongezwa mafuta zikiwa angani.
Jeshi la wanamaji halijathibitisha rasmi hilo likitaja kisa hicho kuw hitilafu.
Sehemu ya helikopta ya jeshi la Marekani yaanguka shuleni Japan
Kulikuwa na wanajeshi watano kwenye ndege ya C-130 na wawili kwenye ndege ya F-18. Mmoja wa wale waliookolewa alikuwa kwenye ndege ya kijeshi, kwa mujibu wa maafisa wa Japan.
Taarifa kwennye mtandao wa Facebook iliyochapiswa na kikosi cha wanamaji ilisema ajali hiyo ilitokea umbali wa kilomita 320 ktoka pwani.
Ndege za Marekani zilikuwa zimepaa kutoka kambi ya Iwakuni na zilikuwa kwenye mazoezi ya kawaida wakati hitilafu hiyo ilitokea.
Waziri wa ulinzi nchini Japan Takeshi Iwaya alisema ndeege tisa za Japan na meli tatua zinashiriki katika oparesehni ya uokoaji.
Mwandishi wa BBC mjini Tokyo anasena kuwa kuongeza mafuta kutoka kwa ndege moja kwenda nyingine hewania na oparesheni hatari hususan wakati inafanywa usiku.
Anasema haijulikani hali ya anga ilikuwa ya aina gani lakini kulikuwa na mawingu mengi usiku na mvua kwennye visiwa vya Japan.
Ndege ya KC-130 ni aina ya ile ya C-130 iliyoboreshwa na hutumiwa kungezea ndege zingine mafuta zikiwa hewani.
Ndege ya McDonnell Douglas F/A-18 Hornet ni ndege ya kivita ya kushambulia na inaweza kubeba makombora ya kila aina na mabomu.
Marekani ina zaidi ya wanajeshi 50,000 walio nchini Japan, zaidi ya 18,000 kati yao wakiwa ni wanamaji.
Marekani ina changamoto na ndege zake nchini Japan . Mwezi Novemba ndege aina ya F/A-18 Hornet ilianguka baharini kusini mwa Okinawa. Marubani wawili waliruka salama na kuokolewa.
Disemba iliyopita sehemu ya ndege ya helikopta ilianguka kwenda shule huko Okinawa na kuzua msukosuko na wenyeji wa kisiwa hicho.
Miaka iliyopita visa kadhaa vya uhalifu vimesababisha kuongezeka kwa malalamiko dhidi ya kambi ya Marekani huko.
Ndege Mbili za Jeshi la Marekani Zagongana na Kuanguka Baharini
0
December 06, 2018
Tags