Ndugai Atoa Ombi Ambalo ni Agizo kwa ATCL

Ndugai atoa ombi ambalo ni agizo kwa ATCL
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ametoa wito kwa Bodi ya Shirika la Ndege la Tanzania, kufanya kazi kwa muda wa saa 24 ili kuweza kuhudumia wasafiri kwa muda wote ikiwa ni pamoja na kuwezesha kupata mapato.


Ndugai amesema hayo leo wakati wa mapokezi ya ndege aina ya Air Bus A220-300 iliyonunuliwa na serikali jijini Dar es salaam.

"Nitoe wito kwa bodi ya Air Tanzania kufanya kazi kwa masaa 24. Tusifanane na bodi ya miaka 4 hadi 5 iliyopita. Tujitahidi sana 'graph' ya mapato iwe ya kupanda", -  Spika Job Ndugai.

Aidha, Spika amewaomba watanzania wote ikiwa mi pamoja na watumishi wa serikali kutumia ndege za ATCL katika safari zao ili kuwezsha shirika kuendelea kuwepo siku zote.

“Tuunge mkono juhudi ili kuwezesha ‘graph’ ya mauzo na mapato ya ndege zetu kuendelea kupanda kila siku na nyie bodi ya ATCL endeleeni kusimamia suala hili ili isiwe kama ile iliyopita,” amesema.

“Bodi iliyopita ilikuwa ikiangalia tu mambo, mapato yanashuka ipo tu, yanaendelea kushuka ipo tu hadi yanafika sifuri haijafanya chochote, jamani tuhakikishe hilo halitokei tena", amesema Ndugai.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad