Rais wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika, TLS, Fatma Karume amesema yuko tayari kuitwa na chama chochote cha siasa nchini kwa ajili ya kutoa elimu ya masuala ya Katiba na sheria za nchi na kusisitiza kuwa msimamo wake hautabadilika.
Fatma Karume ametoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na www.eatv.tv ambapo alijibu swali juu ya kuonekana kwake kwenye kikao cha vyama 6 vya siasa vya upinzani nchini mkutano ambao ulifanyika Zanzibar na kutoa maazimio mbalimbali.
"Mimi nilialikwa na vyama vya upinzani kuwapa mafunzo juu ya Katiba yetu, ili waelewe wanachokijadili kuhusu katiba yetu, lakini pia nikialikwa na CCM kuwaeleza kuhusu Katiba nitawaeleza kila mwanasiasa akitaka kujua katiba yetu tutaishi maisha bora zaidi."
"Kwa hiyo mimi chama chochote kikiniita kiwe CCM, CUF, CHADEMA, ACT -Wazalendo wakiniita kuwaeleza kuhusu Katiba yetu nitaenda kwa sababu ni wajibu wangu," amesema Fatma Karume
Aidha Fatma Karume amesema "CCM hawaniiti kujifunza kuhusu katiba yetu ila wakinialika nitaenda, niko tayari kwenda hata kesho nitaenda na waelewe na msimamo wangu kwenye mafunzo huwa hautabadilika."
SPORT
Masau Bwire ataja sababu ya kuwatolea bunduki
ABOUT US
ABOUT USADVERTISEJOBSTERMS & CONDITIONSCONTACT USFREQUENTLY ASKED QUESTIONS
NETWORK
IPP MEDIAEAST AFRICA RADIOITVRADIO ONECAPITAL RADIOLOKOPROMO
© 2018 East Africa Television Limited. All Rights Reserved