Papa Francis awashusha vyeo makadinali wawili wa kubwa


Papa Francis amewashusha vyeo makadinali wawili kufuatia kukabiliwa na tuhuma za unyanyasaji wa kingono dhidi yao huku mmoja akistafu na hivyo kufanya idadi ya makadinali watatu watakao kosekana kwenye baraza lake linalomshauri. 

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ofisi ya Waandishi Vatican, Mkurugenzi Greg Burke amesema kuwa kwa mujibu wa mkutano uliyofanyika tarehe 27, umeadhimia kadinali George Pell kutoka nchini Australia na mwenzake, Francisco Javier Errazuriz wa Chile kutoendelea kuhudumu kwenye baraza la hilo linalomshauri papa Francis kufuatia tuhuma zinazowakabili. 

“Mnamo mwezi Oktoba, Papa aliwaandikia barua makadinali hao watatu wa kubwa, Kardinali Pell kutoka Australia, Kardinali Errazuriz kutoka Chile na Kardinali Monsengwo wa Kongo akiwashukuru kwa kazi yao,” amesema Mkurugenzi huyo Burke na kuongeza kuwa hawatakuwa tena sehemu ya Baraza na wala Papa hakuwa na majina ya watu watakao chukua nafasi hizo. 

Wawili hao hawakuwepo kwenye mkutano wa mwisho uliyofanyika mwezi Septemba huku msemaji amesema kuwa  Papa aliwaandikia barua wote wawili mwezi Oktoba ya kuwashukuru kwa ushirikiano wao. 

Kadinali Pell, ambaye alikuwa hazina Vatican anakabiliwa na tuhuma za unyanyasaji wa kingono nchini Australia wakati Francisco Javier Errazuriz kwa upande wake akituhumiwa kuficha unyanyasaji aliyofanyiwa mtoto wakati akiwa Askofu Mkuu wa Santiago wote wamekanusha tuhuma hizo. 

Greg Burke amesema kadinali Laurent Monsengwo Pasinya pia ameondolewa kufuatia Askofu huyo wa Kinshasa mwenye umri wa miaka 79 kustaafu majukumu yake pasipo kuhusishwa na tuhuma zozote. 

Hata hivyo amesa hakuna mpango wowote wa kuziba nafasi hizo tatu zilizoachwa wazi katika siku za hivi karibuni. 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad