Polisi Wafanya Ziara ya Kushtukiza Kisiwa cha Mbudya

Polisi Wafanya Ziara ya Kushtukiza Kisiwa cha Mbudya
Kikosi cha Polisi cha Wanamaji jana kilifanya ziara ya kushtukiza katika kisiwa cha Mbudya na kukuta madudu kibao ikiwemo kutokuwepo kwa vifaa vya uokoaji na usalama.

Lengo la kufanya ziara hiyo, ni kuangalia usalama uliopo hasa katika kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka, ambapo Kamanda wa kikosi hicho, ACP Evans Mwijage alisema wamefanya ziara hiyo ili kuangalia shughuli zinazoendela na hawajafanya kwa kisiwa cha Mbudya, bali visiwa vyote vilivyopo kwenye bahari ya hindi.

Alisema wamefanya ziara hiyo ili kujihakikisha usalama kwenye visiwa hivyo, ambapo wanaamini changamoto walizoziona watazifanyia kazi ikiwemo kuhakikisha ajali za mara kwa mara zinazuiwa zisiweze kutokea na kuwepo kwa boti ya usalama mara kwa kisiwani hapo.

Uamuzi huo, umetokana na hali ya usafiri kuelekea kisiwani hapo kuwa sio salama na mamlaka husika kutakiwa kuchukua hatua madhubuti kudhibiti matukio ya ajali za mara kwa mara majini, imeelezwa.

Taarifa za kiuchunguzi  zinaarifu  kuwa ajali za boti kwenda kisiwani humo, zinatokea mara kwa mara lakini zingine zinakuwa haziandikwi kutokana na vifo vya watu hao, kutojumuisha watu maarufu na inapotokea mtu maarufu ndio inaripotiwa kwenye vyombo vya habari.
 
Mbudya ni Moja ya visiwa vilivyopo katika pwani ya Kaskazini mwa jiji la Dar Es Saalam, Maeneo ya Kunduchi.

Ni eneo ambalo ni tengwa kwa lengo la kulinda na kuhifadhi viumbe wa baharini wanaopatikana eneo hilo. Hata hivyo, eneo hilo wageni hawazuiliwi kwenda na kupumzika kisiwani hapo.

Watu wengi hivi sasa wamekuwa wakikitumia kisiwa hiki kama eneo la mpumziko ya weekend na siku nyingine za wiki huku wengine wakienda mbali hadi kupiga kambi ndani ya kisiwa.

Kipo chini ya Wizara ya Uvuvi (Sio Utalii na Maliasili). Kimsingi kuna njia moja kuu ya kuweza kufika hapo ambayo ni kwa njia ya Boti.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad