Rais Magufuli- Aagiza Kikokotoo Cha Zamani Kitumike Hadi 2023

Rais Magufuli- Aagiza Kikokotoo Cha Zamani Kitumike Hadi 2023
RAIS John Magufuli ameamuru mifuko ya hifadhi ya jamii iendelee na kikokotoo kilichokuwa kikitumika kwa kila mfuko kabla ya mifuko hiyo kuunganishwa na kiendelee hadi mwaka 2023 ambapo inakadiriwa kuwa wanachama takriban 58,000 ndiyo watakaokuwa wamestaafu katika kipindi hicho.

Magufuli ameelekeza hivyo leo alipokutana na viongozi wa Shirikisho la Wafanyakazi (TUCTA), vyama shiriki, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (PSSSF & NSSF) na Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii (SSRA), Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Pamoja na uamuzihuo, rais pia alizitaka hifadhi za jamii zipunguze matumizi ya hovyo, ili kuweza kuwalipa wanachama wake vizuri na mapema.

“Tunahitaji watu wetu wapate fedha nyingi walipwe, lakini pia tunahitaji huu mfuko usife, hii ‘formula’ haipo duniani, mtu anamaliza halafu kiwango chake unakizidisha mara nne, hii  haipo,” alisema rais  na kutolea mfano mawaziri na wabunge ambao hulipewa mafao yao yote na kwa wakati mmoja.

Akifafanua, alisema kwamba wakati anashika madaraka kulikuwa na deni la Sh. trilioni 1.2 katika mifuko hiyo na hivyo ilikuwa ni shida kuwalipa.

“Tulipongia madarakani tulikuta deni la trilioni 1.2, serikali yenyewe haijachangia hii mifuko, waliostaafu kwa wakati ule ilikuwa ni shida, kwani hata ile michango ya serikali haitekelezwi,” alisema na kuongeza kwamba mifuko mingine ilikuwa ikiendeshwa kiajabu ikiwa ni pamoja na kuanzishwa miradi ya kiajabu… na miradi mingi ilikuwa ya majengo.

Aliongeza kwamba mifuko ya jamii yote ilikuwa na hali mbaya, kwa sababu haikuwa imeratibiwa vyema ambapo “waendesha mifuko wote walikuwa wanapigana vita, wanagombania wanachama, walikuwa hawapendani…”

Alisema serikali iliamua kuunganisha mifuko hiyo ikiwa ni pamoja na makubaliano kwamba NSSF ifanyiwe marekebisho, hatua  iliyotokana na ombi la muda mrefu la vyama vya wafanyakazi waliotaka kuunganishwa kwa mifuko hiyo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad