Rais Magufuli Akabidhiwa Majina ya Vigogo Serikalini Waliokatiwa Tiketi za Ndege Lakini Hawakusafiri

Rais Magufuli Akabidhiwa Majina ya Vigogo Serikalini Waliokatiwa Tiketi za Ndege Lakini Hawakusafiri
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Tanzania ATCL Ladislaus Matindi, ameeleza tayari ameshamkabidhi Rais Magufuli orodha ya majina ya viongozi ambao walikatisha safari zao za ndege katika shirika hilo licha ya kukatiwa tiketi za serikali.

Akizungumza Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi, amedai wameshatekeleza agizo hilo la Rais Magufuli ambalo alilitoa kwenye hafla ya upokeaji wa ndege mpya ya Tanzania A220-300 aina ya Airbus.

"Majina ya vigogo husika tumeshayakabidhi kwa Rais, tangu tumeelekezwa tulifanyia kazi maelekezo hayo na kisha tukayakabidhi sehemu husika.

“Siwezi kutaja ni vigogo wa kada gani, ukitaka kujua, wasiliana na Ofisi ya Rais wataweza kuwa na majina pamoja na Idara au Taasisi wanazotoka, sisi tumepeleka orodha,” ameongeza Luhindi.

Disemba 23, mwaka huu, alipokuwa akipokea ndege mpya ya tano aina ya Airbus A220-300, Rais Magufuli, aliagiza mishahara ya vigogo wa serikali wanaokadiriwa kufikia 100, ambao wamekuwa wakikatiwa tiketi za ndege na hawasafiri, ikatwe ili kufidia hasara iliyopatikana.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad