Rais Magufuli atema cheche ajira mpya za Polisi

Rais Magufuli atema cheche ajira mpya za Polisi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amelitaka Jeshi la Polisi kusimamia vigezo katika kuajiri Polisi wapya na kuachana na mchezo wa upendeleo ambao umekuwa ukifanyika na baadhi ya watu ambao sio waadilifu ndani ya Jeshi la Polisi.

Rais Magufuli amesema hayo Leo December 21, 2018 kwenye sherehe za Mahafali ya Maafisa wakaguzi wasaidizi wa Polisi yaliyofanyika Kurasini, Dar Es Salaam.

"Natoa wito kwa Jeshi la Polisi kusimamia vigezo vyake katika kuajiri Askari wapya matatizo mengi yaliyomo ndani ya Jeshi la Polisi yalianzia kwenye ajira baadhi ya watu wanaowaajiri hawana sifa za kuwa Askari Polisi," amesema Rais Magufuli.

Pia Rais Magufuli amesema kuwa wale wenye ndugu zao wanaowataka kuwaingiza kwa mgongo wa nyuma wakawe mapolisi wawapeleke pia JKT wakasulubiwe, na pia alifuatilia kweli na anauhakika kuwa hakuna mtu aliyepitishwa kwa sababu hata Naibu Waziri alipeleka watu wake 11 lakini hawakuingia Jeshini.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad