Rais Magufuli Awajia Juu Wanaopinga Stiglers Gorge


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli kwa niaba ya Serikali ameongoza zoezi la kusaini mkataba na kampuni ya Arab Contractors ya nchini Misri, ujenzi mradi wa kufua umeme wa maji wa Stieglers Gorge ambao unatarajiwa kuzalisha zaidi ya megawats za umeme 2100.

Makubaliano hayo yamefikiwa Ikulu Jijini Dar es salaam mbele ya viongozi mbalimbali wa kitaifa wakiwemo Spika wa Bunge, Jaji Mkuu wa Mahakama,  Mawaziri mbalimbali wa nchi pamoja na Waziri Mkuu wa Misri.


"Tumegundua kuwa mradi huu ndio inayoufaa nchi yetu kwa sasa kwasababu chanzo chake ni cha uhakika, kwa tathimini ya awali mradi utazalisha umeme kwa miaka 60 ijayo, na utagharimu trilioni 6.5".


"Mradi huu utaleta manufaa kwa nchi yetu faida nyingine ni kubwa sana, umeme wote tulionao kwa sasa utazidiwa na mradi wa rufiji, na tunategemea mradi huu utakapokamilika gharama ya umeme itapungua sana."


"Nafahamu kuwa wapo watu wanaodai kuwa mradi huu utaharibu mazingira, hiyo siyo kweli hata kidogo. Tunajua kuwa umeme wa maji unasaidia kutunza mazingira, lakini pia eneo litakalotumika ni dogo kulinganisha na ukubwa wa hifadhi," amesema Rais Magufuli.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mkulu MUNGU Akuhifadhi.. Umeiandika Historia ya nchi yetu kwa Dhahabu. Ntaomba mama Ndalichamo aianzisbe kitabu mashuleni at different levels.
    Ntakuwa Mzaledo kwa Nchi YANGU. Moja ya mifano NI ukombozi huu WA kiuchumi na Miu do mbinu na Huduma karibia Miaka 60 baada ya uhuru Midu. E JPJM amethubutu na amefanya kweli.

    Allah Akuhifadhi na Inshallah akupe Afya Uendelee KUTUTUMIKIA.

    Wapiga KELELE MUNGU washindwe A Walegee.. Wasiokuelewa MUNGU awape ufahamu WA kuelewa kama Si WAO BASI WATOTO ZAO NA WAJUKUU zao

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad