Rais was TFF Afunguka Kuhusu Mdhamini wa Nje Atakayedhamini Ligi Kuu

Rais was TFF Afunguka Kuhusu Mdhamini wa Nje Atakayedhamini Ligi Kuu
Rais wa Shirikisho la soka nchini (TFF), Wallace Karia amevunja ukimya na kuweka wazi kuwa wapo mbioni kumalizana na mdhamini wa ligi kuu soka Tanzania bara msimu huu wa 2018/19.

Karia ameweka wazi kuwa wamekuwa kimya kwa muda mrefu kwa kuhofia kuharibu mipango ambayo wanaendelea nayo lakini sasa wamefikia pazuri na muda wowote wanaweza kupata mdhamini mkuu wa ligi.

''Kuhusu mdhamini tumefikia pazuri, hivi karibuni tulikuwa mjini Durban Afrika Kusini, tumeongea na kampuni moja ambayo inafanya shughuli zake hapa nchini kwahiyo tupo kwenye hatu nzuri ya kupata mdhamini'', amesema Karia.

Karia amesema sababu za kujitoa mdhamini aliyekuwepo kampuni ya Vodacom ni kwasababu walishusha kiwango cha fedha na wao kama TFF hawakuwa tayari kuendelea nao kulingana na thamani ya ligi hivyo wakaachana.

Ligi kuu soka Tanzania bara ambayo ipo katika raundi ya 13 inaendelea bila kuwepo kwa mdhamini mkuu hivyo hata zawadi ya bingwa bado haijawekwa wazi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad