Ratiba ya Simba Ligi kuu yabadilishwa tena

Ratiba ya Simba Ligi kuu yabadilishwa tena
Bodi ya Ligi (TPLB) kupitia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imetangaza mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba vs Singida United kupigwa Disemba 29 badala ya 30.

Mabadiliko yamekuja kutokana na mmiliki wa Uwanja kusema utakuwa na matumizi ya kiserikali kwa siku za Disemba 30 na 31.

Mechi hiyo imerudishwa nyuma ambapo sasa itapigwa majira ya saa 1 kamili za usiku kwenye Uwanja ulele wa Taifa.

Wakati kabla ya mechi hiyo kupigwa, kikosi cha Simba kipo mawindoni kujiandaa na mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayopigwa dhidi ya Nkana Red Devils kwenye Uwanja wa Taifa, Jumapili ya wiki hii.

Simba ianenda kucheza mchezo huo ikipaswa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 tu na isiruhusu nyavu zake kuguswa ili kufanikiwa kutinga hatua inayofuata.

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Enter your comment...TFF amashisheni clabu zinazoshiriki ligikuu ziwe na viwanja vyake cyo kuazima azima leo hihi timu inasongezwa mbele kisa mwenye uwanja amepata shughuli kikwely inakera sana

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad