Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema anatamani kuwa kiongozi wa dini kuliko kazi ya Ukuu wa Mkoa.
Makonda alitoa kauli hiyo ijini Dar es Salaam jana, alipozungumza na viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali na kuongeza kuwa wakati akiwa chuoni aliandaa semina za dini ambazo zilihudhuria na wanafunzi wengi.
“Ukiniiuliza kazi gani ninayoipenda nadhani nitakwambia hii ya kuwa kiongozi kwa dini kuliko ya Ukuu wa mkoa. Napenda kukaa katika nyumba ya bwana siku zote za maisha yangu,”alisema Makonda.
Alisema kitendo cha kukusanyika kwa viongozi hao wa dini kutoka madhehebu mbalimbali kwake ni utukufu kutoka kwa Mungu.
“Nimeona nianzishe utamaduni wa kukutanisha viongozi wa dini. Mwaka 2012 mkutano nilifanya mkutano wangu wa mwisho wa 18 na Mchungaji Christopha Mwakasenge katika viwanja vya vyuo vya Ushirika ambapo uwanja mzima ulijaa,”alisema.
Naye Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe, alisema wengi wanajua kwamba yeye ni mkosoaji lakini hawajui kuwa pia ni msifiaji.
“Nampongeza Makonda kwa wito huu na alitaka kufahamu kuwa kama nitakuja au la, nilimwambia kusudi la hafla hii ni kuujenga mwili wa Kristo, sasa kama ni mtumishi wa Mungu sitaki kujenga mwili wa Mungu nitajenga kitu gani,”alisema.
Alisema kuwa amekuwa katika huduma kwa miaka 30, hajawahi kuona kusanyiko la watumishi wa Mungu kutoka madhehebu mengi mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa kukusanya watumishi wa Mugu kutoka madhehebu mbali mbali ni jambo linalohitaji upako.
RC Makonda Atoa Ujumbe Mzito Kwa Viongozi wa Dini....Kakobe Afunguka Sakata la Kuitwa Mkosoaji
0
December 27, 2018
Tags