Sababu za Tanzania Kuchemka Beach Soccer Zaanikwa


Kocha wa timu ya taifa ya soka la ufukweni Boniface Pawasa ameweka wazi sababu za timu yake kufanya vibaya katika fainali za beach soccer kule Misri.

Tanzania imepoteza mechi zake zote za kundi lake ambapo ilikuwa inashiriki kwa mara ya kwanza.

“Kitu cha kwanza ni uzoefu na hii inatokana na kwamba hatukuwa na michezo mingi ya kutosha lakini wenzetu licha ya kuwa na uzoefu wana ligi kwenye nchi zao.”

“Tumecheza na nchi ambazo zina mifumo ya ligi ina maana wachezaji wao wamechaguliwa kutoka kwenye ligi za beach soccer ambazo zinaendelea kwenye nchi zao lakini pia uzoefu wa nchi hizi kwenye mashindano haya ya AFCON.”

“Nchi tulizochezanazo ni Senegal, Nigeria na Libya, Libya ina uzoefu wa miaka 7 kucheza mashindano haya. Senegal imekuwa ikishiriki mashindano haya kwa miaka 12 hali kadhalika kwa Nigeria. Halafu Nigeria na Senegal ni timu ambazo mwaka jana zilicheza fainali Senegal akawa bingwa.”

“Lakini tumefanikiwa kujifunza kuanzia wachezaji hadi benchi la ufundi na kumekuwa na mabadiliko mechi hadi mechi ukiachilia mechi yetu dhidi ya Senegal ambayo tulizidiwa kwa kila kitu mbinu na ubora wa mchezaji mmoja mmoja.”

“Tunahitaji kuwa na ligi endelevu na yenye support. Tumekuja natimu ambayo ilikuwa na maandalizi inafika wakati inakosa hata maji ya kunywa, wachezaji wanakosa hata nauli ya kutoka mazoezini kurudi nyumbani.”

Shafii
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad