Nahodha wa Real Madrid, SergioRamos amesema kuwa kila mmoja angependa kuwa na kocha kama Jose Mourinho ndani ya timu yake kwakuwa anakiwango cha hali ya juu, huku hakusita kusisitiza kuwa nilazima kumheshimu meneja waliyenae kwa sasa, Santiago Solari.
Image result for sergio ramos and Mourinho
Mourinho ambaye ameiyongoza Real kuanzia mwaka 2010 hadi 2013 ametimuliwa kazi Manchester United siku ya Jumanne baada ya kuhudumu kwa miaka miwili na nusu ndani ya OldTrafford.
Real ilimtimua meneja wake Julen Lopetegui mwezi Oktoba kabla ya Solari kurithi mikoba yake ambaye anajiandaa kukabiliana na Al Ain kwenye mchezo wa fainali ya klabu bingwa duniani.
“Tuna miaka mitano tangu Mourinho aondoke na bado tunamzungumzia Mourinho, kwa nini ?,” ameuliza Ramos.
Sergio Ramos ameongeza kuwa “Yeye ni kocha wa kiwango cha hali ya juu kwa hiyo kilamtu anamuhitaji. Real Madrid imeshinda kila kitu hivyo ni lazima tumheshimu meneja tuliyenaesasa.’’
“Hatuna Mourinho,tuna Santiago Solari. Tunakwenda kuangalia kama tutafanikiwa kushinda taji na pengine baada ya hapo tutazungumzia kuhusu Mourinho, nisingependa kuwa sehemu ya tetesi za ujiowake.’’
“Unadhani kwamba kwasababu mimi ninahodha basi naweza kusema nani atakuja kuwa kocha Real Madrid?. Ni maamuzi ambayo mimi huwa sina chochote cha kufanya.”
Real imetinga hatua ya fainali yakombe la dunia ngazi ya klabu baada ya nyota wake Gareth Bale kupiga hat-trickmchezo uliyomalizika kwa jumla ya mabao 3-1 dhidi ya Kashima Antlers siku yaJumatano.
Sergio Ramos: Mourinho ‘Ni Kocha wa Kiwango cha Juu, Kila Mtu Anamuhitaji’
0
December 22, 2018
Tags