Serikali kuanza kupima DNA

Serikali kuanza kupima DNA
Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale, Hamimu Gwiyama amesema serikali wilayani humo, itaanza kupima vinasaba kati ya mtoto na mwanamume aliyemuoa mwanafunzi ili kubaini kama ndiye baba halisi.


Kauli hiyo imekuja ikiwa ni baada ya kujulikana kuwa wanafunzi wanaoacha shule kwa kupata ujauzito kukataa kuwataja wanaowapa mimba kwa madai hawawafahamu.

“Wanafunzi wengi waliopata mimba sasa wameolewa, lakini wanapohojiwa kujua aliyewapa mimba, wanadai hawamjui au hawamkumbuki, sasa polisi watafanya uchunguzi na kuwahoji wote wawili kujua ukweli itakapokuwa ngumu tutawapima vinasaba,” Gwiyama.

Baada ya kuwepo na rekodi ya mimba zaidi ya 160 za wanafunzi kwa kipindi cha miaka mitatu, ndani ya wilaya hiyo, Mkuu huyo wa wilaya amesema kwamba Serikali imeamua kuwasaka hata ambao wameolewa ili kubaini kama wanaume hao ndiyo waliokatisha ndoto zao za masomo.

Mbali na hayo, amesema waraka wa Elimu namba 5 wa mwaka 2011 unaoruhusu mwanafunzi kufukuzwa shule baada ya kuwa mtoro kwa siku 90, umechangia wazazi wengi kuwakatisha masomo wanafunzi na kuwaoza.

“Tumeanza operesheni ya kuwasaka wote walioacha shule haijalishi ni baada ya miaka mingapi, bali wote walioacha shule tutawachukulia hatua. Lengo la operesheni hii ni kumaliza tatizo la mimba, tuwajengee hofu wanaume wanaowaoa wanafunzi,” Gwiyama.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nilifikiri serikali au taasisi husika ingefanya utafiti wa kisayansi kubaini kinachopelekea ongezeko la mimba za utotoni halafu iyafanyie kazi matokeo ya utafiti huo

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad