Serikali ya Burundi Yaitimua Ofisi ya Haki za Binadamu ya UN na Kuihamuru Iondoke Nchini Humo

Serikali ya Burundi Yaitimua Ofisi ya Haki za Binadamu ya UN na  Kuihamuru Iondoke Nchini Humo
Serikali ya Burundi imeliamrisha baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kufunga ofisi na kuondoka nchini humo ndani ya meizi miwili, kwa mujibu wa wizara ya mashauri ya nchi za kigeni na Umoja wa Mataifa waliozungumza na AFP.

"Serikali wa Burundi imekuwa ikionyesha ukali dhidi jamii ya kimataifa," AFP imeunukuu Umoja wa Mataifa.

Burundi ilisusia mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwezi Novemba ambao ulilenga kuzungumzia mzozo wa kisiasa unaoendelea nchini Burundi.

Mwaka 2007 Burundi ilijitoa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Jinai baada ya mahakama hiyo kuanzisha uchunguzi kuhusu dhuluma nchini humo.

Ghasia zilizuka chini humo mwaka 2015 wakati Rais Pierre Nkurunziza alitangaza kuwa angewania muhula wa tatu.

Mzozo huo wa kisiasa ulisababisha mamia ya watu kuuawa na zaidi ya 400,000 kukimbia nchi kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad