Serikali ya Uganda Yafungia Mitandao

Serikali ya Uganda Yafungia Mitandao
Serikali chini Uganda kupitia Tume yake ya mawasiliano (UCC) imefungia mitandao inayoonyesha picha za ngono kwenye simu nchini humo.


Takriban tovuti 25 zinazoonyesha video hizo haziwezi kufunguka kwa sasa nchini humo kutokana na zuio hilo.

Mamlaka hizo zilifikia uamuzi wa kuzifungia baada ya kugundua kuwa tovuti hizo ni miongoni mwa tovuti 100 zinazotazamwa sana Afrika Mashariki.

Mwenyekiti wa Kamati ya kupambana na video za ngono nchini humo, Dr Annette Kezaabu amesema zuio hilo la tovuti kubwa za video za ngono limesaidia kushusha idadi ya watu wanaotazama kwa kipindi kifupi tangu lilipotangazwa.

"Mpaka sasa tunaendelea na mchakato wa kupitia majina mengine ya tovuti ambazo tutazifungia kutokana na video hizo. Tunafahamu kwamba watu watafungua tovuti zingine lakini huu ni mpango endelevu," amesema Dr Annette.

Zuio hilo nchini Uganda limekuja siku chache baada ya Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani nchini Kenya kuiomba serikali ya nchi hiyo kufungia tovuti za video za ngono kwa lengo la kupunguza ongezeko la mimba za utotoni.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad