Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga amebainisha kufungwa kwa muda akaunti za benki 191 zinazomilikiwa na wakulima wa Korosho lengo likiwa ni kuhakiki wamiliki wa korosho hizo ambazo zilinunuliwa na serikali.
Waziri Hasunga amesema hatua hiyo imekuja wakati ikiwa imeshaingiza Sh 3.8 bilioni kwenye akaunti hizo katika mfululizo wa uhakiki na ulipaji wakulima.
Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga amesema “hatua hii ya kufunga akaunti hizi kwa muda ni muhimu ili kupisha uhakiki kwa sababu utaratibu unataka mkulima aliyeuza zaidi ya kilo 1,500 za korosho aonyeshe shamba lake lilipo kwa timu yetu ya uhakiki.”
Mpaka sasa tayari Shilingi bilioni 206 zimeshalipwa kufikia Desemba 27 kati ya hizo, Sh 188.378 bilioni zilikuwa zimewafikia wakulima kabla ya sikukuu ya Krismasi.