Simba Wahimizwa Kutumia Vema Uwanja wa Nyumbani


Wachezaji wa Simba wametakiwa kujiandaa kisaikolojia kwa kutumia vema Uwanja wa nyumbani kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Hayo yamesemwa na Mchezaji wa zamani wa Taifa Stars na klabu ya Simba, Madaraka Selemani, na kusema kuwa Simba kufanya hivyo ili wanufaike kama ambavyo walifanikiwa kwa Mbabane Swallows ya Swaziland kwa kuichakaza kwa jumla ya magolo 4-1 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mkongwe huyo ambaye alitamba kwenye soka la miaka hiyo ana imani Simba wakipambana vema Dar es Salaam basi katika michezo ya marudiano kama wataanzia nyumbani hawatapa tabu.

"Simba wanapaswa kujipanga vema na haswa wajitahidi kutumia zaidi faida ya uwanja wa nyumbani kwani itawasaidia kupenya kirahisi kwa mechi ambazo wataanzia Dar es Salaam" alisema Seleman.

Katika kundi D Simba ipo na moja ya klabu ambazo ni Al Ahly ya Misri na AS Vital ya Congo ambazo zote ni moto wa kuotea mbali.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad