Simba Wapigwa na Mashujaa 3-2.... Watupwa Nje Kombe la Shirikisho



Klabu ya soka ya Simba imeng'olewa katika michuano ya

shirikisho (Azam Sports Federation Cup) baada ya kupokea kichapo kutoka kwa Mashujaa FC .

Simba walikuwa wa kwanza kuandika bao dakika ya 18 kupitia kwa Paul Bukaba akimalizia shuti lililotemwa na mlinda mlango wa Mashujaa baada ya kutema shuti lililopigwa na Said Ndemla.

Kipindi cha pili Mashujuaa walisawazisha bao dakika ya 48 kupitia kwa Said Hamisi, bao la pili wakaandika dakika ya 57 kupitia kwa Jeremiah Josephat na msumari wa mwisho ukikomelewa na Rashid Athumani dakika ya 90 na mabao yote hayo ni kutokana na uzembe wa safu ya ulinzi na mlinda mlango Deogratius Munish 'Dida'.

Bao la pili la Simba liliandikwa dakika ya 60 baada ya faulo iliyopigwa na Clytous Chama aliyeingia dakika ya 60 akichukua nafasi ya Abdallah Seleman na kufungwa na Paul Bukaba dakika ya 80.

Mlinda mlango wa Mashujaa amekuwa ni shujaa kwa kuokoa mashuti ya washambuliaji wa Simba ambao mpaka mpira unaisha  wamecheza kona 10, huku mashuti mawili ya Rashid Juma na Mzamiru Yassin yakigoga mwamba.

Kikosi cha Simba kilikuwa na sura nyingi mpya ambazo zimekuwa hazipati nafasi kwenye kikosi cha kwanza ikiwa ni pamoja na kinda Abdallah Seleman, Asante Kwasi, Deogratius Munish.

Simba imeondolewa katika michuano hiyo kwa msimu wa pili mfululizo, ambapo msimu uliopita iliondolea katika hatua hii kwa kufungwa na Green Warriors kwa mikwaju ya penati 4-3.

Inabakiza nafasi mbili pekee za kupata tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao, ambazo ni Ligi Kuu Tanzania Bara endapo itaibuka bingwa pamoja na michuano ya Klabu Bingwa Afrika endapo itashinda ubingwa huo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad