Solskjaer ni chaguo sahihi Man United


Manchester United ilikuwa imeachana na utamaduni wake, tangu Sir Alex Ferguson ameondoka walijaribu walikuwa wanajaribu kupata mtu ambaye atakuja kuindesha na kuijenga United katika misingi ya ki-manchester United lakini bahati mbaya watu wote waliokuja walikuwa na falsafa zao.

Moyes sote tunamjua alipata mafanikio akiwa na Everton lakini Everton sio kariba ya Manchester United na yeye pia alikuwa anataka kupata mafanikio atambulike miongoni mwa makocha bora. Inahitaji muda United haina muda huo tena kama ilivyokuwa kwa Ferguson.

Van Gaal wakamleta kwa ajili ya kupata kilichobora kutoka kwake kwa sababu tayari alisha-prove ni kocha bora ambaye alishapata mafanikio Barcelona, FC Bayern, Ajax, lakini pia utamaduni wa Manchester ukamshinda hakufanikiwa kufikia malengo.

Mourinho uzoefu aliokuwanao kwenye EPL wakafikiri angeweza kufanya kitu ndani ya muda mfupi kuirudisha United katika level zile watu walizotarajia yeye pia akaja na mipango yake akawaondoa watu wote wa benchi la ufundi waliokuwa na utamaduni wa timu akaja na watu wake wapya na akaanza upya mwisho wa siku imekula kwake.

Ujio wa Ole Gunnar Solskjaer naiona sio ujio wa mtu aliyepata mafanikio huko kwingine lakini wanamleta mtu ambaye anaujua utamaduni wa Man United. Mchezaji ambaye amekaa chini ya Sir Alex Ferguson na kama walivyosema ni mkataba hadi mwishoni mwa msimu wanategemea kuona anaweza kufanya kitu gani ili kama atafanya vizuri wampe mkataba wa muda mrefu.

Nilicbokiona Solskjaer ataweza kurudisha ile morali kwa sababu watu wanaoijua Manchester tangu zamani wanajua ni timu ya aina gani, hawana wachezaji wenye majina makubwa wao wanacheza kwa morali kwa hiyo huyu kocha atawaambia wachwzaji wapo katika timu ya aina gani.

Kwa mfano ukimfuatilia Patrice Evra post zake kwenye mitandao ya kijamii anaielezea Manchester kuwa ni klabu ambayo ina style yake na utamaduni wake ambao yeye hauoni. Kwa hiyo bodi ya wakurugenzi wameona hilo Solskjaer amekaa United takribani miaka 10 ni mchezaji ambaye hajapata mafanikio makubwa kama nilivyosema mwanzoni nadhani wamemleta ili awaambie wachezaji wao walikuwa wanafanya nini kwenye dressing rooms wakiwa chini ya Ferguson.

Wamemrejesha pia Mike Phelan huyu alikuwa chini ya Ferguson kwa hiyo utaona watu wanaoletwa ni wale wanaoujua utamaduni wa Manchester United. Phelan ni mtu ambaye amekaa kwa muda mrefu Manchester lakini aliondoka baada ya ujio wa makocha wapya waliokuja kuchukua nafasi ya Ferguson.

Kwangu mimi naona ni mamauzi sahihi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad