Tamasha la Fiesta Laacha Historia Dar RC Makonda Amtaja Ruge Kuwa Shujaa

Tamasha la Fiesta Laacha Historia Dar RC Makonda Amtaja Ruge Kuwa Shujaa
MSIMU wa Fiesta 2018 uliokuwa na Kaulimbiu ya Vibe kama Loteee, licha ya awali kutaka kuingia dosari kwa kutofanyika jijini Dar mwaka huu, hatimaye tamasha hilo limefanyika na kufunika mwanzo-mwisho, Ijumaa Wikienda lilikuwepo linakupa A-Z lilivyokuwa.

Tukio hilo la kihistoria lilihitimishwa rasmi kwenye Viwanja vya Posta vilivyopo Kijitonyama jijini Dar, palipofurika, usiku wa kuamkia jana ambapo lilinoga ile mbaya tofauti na wengi walivyofi kiri.


Katika tamasha hilo, pamoja na kupambwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali wa Bongo Fleva, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipanda jukwaani na kuwapa ofa mashabiki waliofurika kwenye tamasha hilo si tu kwa kujirusha hadi asubuhi, bali aliwapa ruhusa ya kujirusha kwenye tamasha hilo kwa siku tatu mfululizo usiku na mchana kama wataweza.

MAKONDA AMTAJA RUGE KAMA SHUJAA Sambamba na hilo, Makonda alipopanda jukwaani alielezea simanzi yake kwa kufanyika tamasha hilo bila uwepo wa mmoja wa waanzilishi wake, Ruge Mutahaba aliyeko nchini Afrika Kusini kwa matibabu huku hali yake ikiwa na usiri mkubwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad