Tanzania yaenda AFCON, Kaseja afunguka

Tanzania yaenda AFCON, Kaseja afunguka
Timu ya Taifa ya Tanzania ya Soka la Ufukweni, imeondoka leo alfajiri, Desemba 5, 2018 kwenda nchini Misri kwenye fainali za Afrika za soka la ufukweni zinazotarajia kuanza Desemba 8 mpaka14, 2018.

www.eatv.tv imefanya mahojiano na Juma Kaseja ambaye ni miongoni mwa wachezaji waliosafiri na timu kwenda Misri na amesema kwa uzoefu wa makocha Boniface Pawasa na  Talib Hilal anaamini watafanya vizuri katika michuano hiyo.

''Nina imani kubwa na uwezo wa kocha Talib Hilal, amekuwa mwalimu wa soka la ufukweni kwa muda mrefu akiifundisha timu ya taifa ya Oman hivyo na alivyokitazama kikosi na aina ya mipango yake ilivyo nadhani tutafanya vizuri'', amesema.

Kwa upande wa kikosi Kaseja amesema wachezaji wengi walioitwa ni wale wenye uzoefu na soka la ufukweni na wamekuwa wakifanya vizuri kwenye michuano ya ndani ikiwemo yale mashindano ya Copa Dar es salaam ambayo yamemalizika hivi karibuni kwa Tanzania kuibuka bingwa mbele ya nchi za Malawi, Uganda na Shelisheli.

Aidha Kaseja ameweka wazi kuwa wapo kundi gumu la B, lenye timu za Senegal, Nigeria na Libya, lakini kwenye mchezo wa soka lolote linawezekana na wao watahakikisha wanapata ushindi. Kundi A lina timu za Egypt, Morocco, Ivory Coast na Madagascar.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad