Tobaa! Kati ya Walioleta Mahari ni Kaka wa Mchumba na Nishatoka Naye Kimapenzi


Jamani I'm confused, naombeni ushauri.

Kuna kaka mtu mzima (early 40s) alikuwa BAE wangu nikiwa chuo kwa miaka 2. Yy alikuwa c mwanachuo wakati huo.

Lkn nilipomaliza chuo nilimpiga kibuti, ili niangalie maisha baada ya chuo.

Ktk kupita huku na kule mwaka jana january nikakutana na mkaka kijana (32yr), mm nikiwa na 24yrs tu. Mtoto wa kike nikaona huyu nigandane naye na kwakuwa ananipenda tukaanza michakato ya kuoana.

Niliwapa taarifa wazazi wangu posa ikaletwa na tarehe ya mahari ikapangwa. Siku mahari inaletwa mmoja wa wanafamilia ktk utambulisho wa wale wageni akawa yule BAE wa chuo.

Alitambulishwa kama kaka wa muoaji (mchumba). Tobaa! Mtoto wa kike huko ndani kijasho kikanishuka (kwa mila zetu muolewaji unatakiwa kuwa chumbani siku mahari inaletwa, ila unakuwa unapewa taarifa ya kila kinachojiri, au hata ukiweza waweza kuwa kwenye kidirisha unafuatilia yanayoendelea). Kwahiyo yy hakuniona

Nimekosa raha kabisaa! Naombeni ushauri, niendelee na mchakato wa kuolewa na huyu kaka ama nisitishe?

Ninapositisha mchakato nitatoa sabb gani kwa mchumba na wazazi?

Nikiolewa, yule kaka mtu tutatazamana kwa jicho gani? Kutakuwa na heshima kweli?
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad