"Tumejipanga uchaguzi wa 2020" - Sirro

"Tumejipanga uchaguzi wa 2020" - Sirro
Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon N. Sirro amesema Jeshi hilo limejipanga vya kutosha kusimamia usalama katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika na ule wa 2020.

Kamanda Sirro ameyasema hayo leo Disemba 21, 2018 katika mahafali ya kuhitimisha mafunzo ya maofisa na wakaguzi wasaidizi wa polisi, ambapo ameweka wazi kwamba hawatatoa nafasi kwa mtu yeyote kuhatarisha amani ya nchi ya Tanzania.

“Tunaendelea kutekeleza maagizo yako ya mara kwa mara na tunajua kuwa kuna uchaguzi 2019 na 2020 na tumejipanga vizuri kuhakikisha uchaguzi unakwenda sawa,” amesema.

Kwa kutilia mkazo kauli ya IGP Sirro, Rais Magufuli amelikumbusha Jeshi hilo kuhakikisha kunakuwa na usala wakati wa uchaguzi.

“Ninawakumbusha jeshi la polisi kuwa tumebakisha siku chache kuingia mwaka 2019 ambao ni wa uchaguzi wa serikali za mitaa kama tunavyofahamu chaguzi nyingi zinaleta fujo hivyo mkasimamie na kuhakikisha kunakuwa na usalama," amesema Rais Magufuli.

Mbali na hayo, Rais Magufulia amelitaka jeshi la polisi kukiangalia kitengo cha fedha na kwamba yapo malalamiko mengi ikiwemo suala la fedha  zinazotumwa na serikali kutowafikia wahusika.

"Ninataka Jeshi la Polisi pamoja na majeshi mengine pasiwe na malalamiko lazima kila mmoja afaidike na uaskari wake,” ameongeza Rais Magufuli.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad