Ubunge wa Mtolela Wapingwa NEC Yafunguka Kupokea Barua

Ubunge wa Mtolela Wapingwa NEC Yafunguka Kupokea Barua
Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini (NEC), imetangaza kupokea rufaa ya Ngulangwa Mohamed Mshamu, wa CUF, akipinga kutangazwa kushinda bila kupingwa kwa Mgombea Ubunge wa Chama Cha Mapinduzi CCM, katika Jimbo la Temeke Abdallah Mtolea.

Kwa mujibu wa tume hiyo, walipokea taarifa ya kupingwa kwa ushindi wa Mtolea mara baada ya kutangazwa na msimamizi wa uchaguzi lakini wamedai suala hilo liko nje ya uwezo wao.

"Tume ilipokea malalamiko kwa Ngulangwa Mshamu (CUF) akipinga uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Temeke kumuondoa kwenye orodha ya wagombea Ubunge na kumtangaza mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Abdallah Ally Mtolea  kuwa amepita bila kupingwa."

Aidha taarifa hiyo imesema "kwa mujibu wa kifungu cha 44 cha Sheria ya taifa ya uchaguzi, mgombea akitangazwa kuwa amepita bila kupingwa NEC haina mamlaka juu ya uamuzi wa msimamizi wa uchaguzi''.

November 15 mwaka huu akiwa Bungeni Mtolea alitangaza kujivua wadhifa wake wa ubunge kwa kile alichokidai kuwa chama chake cha CUF kugubikwa na mgogoro.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad