“Ugomvi Wa Clouds na Wasafi Haunihusu Naangalia Pesa”-Linah


Msanii wa Bongo fleva Linah Sanga amefungukia tuhuma za kuonekana kuisaliti Clouds Media Baada ya kuonekana akiwa na Wasafi Festival ambapo amekuwa akipiga shoo mbali mbali.

Linah Sanga alianzia safari yake ya kimuziki katika Nyumba ya vipaji Tanzania (Tanzania House of Talents) na kupatia mafanikio makubwa lakini msanii huyo hajaonekana upande huo kwa muda mrefu.

Baada ya kuonekana zaidi na Wasafi Festival Linah ameibuka na kujitetea kuwa yeye hajamind ugomvi uliopo kati ya Wasafi na Clouds yeye yupo kikazi zaidi yeye Kama Msanii anaangalia maslahi yake huku mabifu yao yakiwa hayamuhusu.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Linah Sanga alifunguka haya Kuhusu kuisaliti Clouds na kuhamia Wasafi:

Wakati nipo THT nilifundishwa kuwa mimi ni mfanyabiashara na Mimi ni brand hivyo siangalii nafanya wapi kazi as long as naingiza mkwanja halafu isitoshe hayo maugomvi mimi hayanihusu mimi naangalia pesa ambayo naingiza katika kazi ninayopewa”.

Linah Sanga pia alifungukia picha zake zilizosambaa kwenye mtandao wa kijamii zilizomuonyesha akiwa amevaa vinguo vifupi na kuonekana na Neil I mkubwa tofauti na anavyojiweka kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo amesisitiza picha zile zimetoka vile kutokana na kwamba zilipigwa alipokuwa anatembea.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad