Umoja wa Mataifa wautambua rasmi muziki wa Reggae

Muziki wa Reggae umetambuliwa rasmi na Umoja wa Mataifa kwa kuongezwa kwenye hazina za kiutamaduni za dunia, ambazo zinahitajika kulindwa na kutangazwa zaidi duniani.

Maamuzi hayo yamefikiwa hivi karibuni, baada ya ombi la muda mrefu kutoka Jamaica ambalo liliwasilishwa na Waziri wa Utamaduni, Olivia Grange , katika mkutano wa Umoja wa Mataifa kutaka kuutambuliwa rasmi kwa muziki huo.

Muziki wa reggae sasa utaungana na tamaduni zingine duniani ambazo zimetambuliwa na Umoja wa Mataifa, ukiwemo mchezo wa Hurling.

Nalo Shirika la UNESCO, limesema kuwa mchango wa muziki huo kimataifa umekuwa ukijadili masuala mbali mbali ya haki, amani, upendo, utu na kuleta nguvu kwenye ufahamu wa ubongo.

Katika historia, muziki wa reggae ulianzishwa miaka ya 1960’s baada ya kuunganishwa kwa mapigo ya muziki wa aina ya Ska na Rock stead.

Muziki huo ulipata umaarufu zaidi duniani, kupitia bendi ya muziki ya ‘Toots and the Maytals’, kisha The Wailers iliyoanzishwa na Bob Marley, Peter Tosh na Bunny Wailers.

Mpaka sasa baadhi ya nchi duniani bado zinauenzi muziki huo kwa asilimia kubwa, ikiwemo Jamaica hii ikiwa ni tofauti kabisa na nchi za mataifa ya Ulaya  na Afrika.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad