UN: Ongezeko la Joto Sasa ni Tishio kwa Binaadamu

UN: Ongezeko la Joto Sasa ni Tishio kwa Binaadamu
Umoja wa mataifa umeonya kuwa ongezeko la joto sasa ni tishio kwa binadamu kuliko ilivyokua huko miaka ya nyuma.

Akizungumza katika mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya hali ya hewa huko Poland, kiongozi wa Umoja wa mataifa kuhusu hali ya hewa, amesema kuwa mwaka huu ni miongoni mwa miaka minne yenye joto zaidi duniani.

Wawakilishi kutoka sehemu mbalimbali duniani wanatarajia kuleta mabadiliko kwa kuanza kufanyia kazi mkataba wa hali ya hewa wa Paris.

Mkutano umeanza rasmi mapema Jumatatu, ni mkutano mkubwa wa hali ya hewa na tabia nchi kufanyika tangu ule wa Paris wa mwaka 2015.

Wakati huo huo Benki ya dunia, imetoa dola bilioni 200 zilizoelekezwa kwa nchi zinazochukua hatua za kupambana na mabadiliko ya tabia nchi kwa miaka mitano ijayo.

Rais wa umoja wa mataifa katika masuala ya hali ya hewa, Maria Esposa amesema kuwa jitihada za haraka zinahitajika.

''Tulipoanza na mkutano wa masuala ya hali ya hewa mwaka 1995, ni kama tulikua tukipanga maisha ya baadae, na tulikua tukizuia kuharibika kwa hali ya hewa, lakini sasa tunaishi ndani yake, sasa tunatakiwa tujikomboe haraka , na jamii inatakiwa ikubaliane na mabadiliko haya.

Esponsa, amesema pia wajumbe wamekutana ili kujadili namna ya kujikomboa na mabadiliko hayo ya tabia nchi, na kuhakikisha makubaliano ya Paris yanafanyiwa kazi.

Viongozi wanne wa umoja wa mataifa waliomaliza muda wao, na wazungumzaji wakuu kuhusu hali ya mabadiliko ya tabia nchi, walitoa tamko la kutaka jitihada za haraka kuchukuliwa ili kuzuia mabadiliko haya ya kasi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad