Usimdharau Mtu Usie Mjua...Soma Kisa Hichi cha Diamond Platnumz


Mwaka 2005 Diamond alisafiri kwenda Tanga kuomba kuperform kwenye show ya Q-Chilla. Mabaunsa wakamtimua..... Alipojaribu kuwaelewesha wakambeba juu juu na kumchania Tshirt na kumtupa nje. Bahati nzuri Q-Chilla alijulishwa kuhusu purukushani hizo, na alipoenda akasema aruhusiwe kuingia na apewe nafasi ya kuperform

Leo wale mabaunsa pengine wanatamani kuwa mabaunsa wa Diamond lakini haiwezekani.
Joseph Kabila aliwahi kuelezea kuwa kipindi anaishi Tanzania aliwahi kushushwa kwenye basi porini huko mkoani Iringa kwa sababu hakuwa na nauli ya kutosha. Alijaribu kumuomba konda amshushe angalau mahali penye mji lakini hakumuelewa na akamtelekeza porini. Akatembea kwa mguu hadi Nyololo ndipo akapata msaada. Leo yule konda pengine anatamani kupata nafasi walau ya kumuomba msamaha Kabila lakini haiwezekani. Hakujua kama aliyemshusha porini angekuja kuwa Rais wa nchi

Mwanzoni mwa miaka ya 1980's Meneja wa hoteli moja ya kitalii huko Hangzhou, alimnyima kazi Jack Ma. Baadaye Jack Ma alianzisha kampuni ya Alibaba na kumuajiri mtu huyo aliyemnyima kazi kuwa Meneja masoko wa online auction hosting ya Alibaba.
Maisha ni kama sarafu iliyotupwa angani, huwezi kutabiri itadondokea upande upi. Hakuna anayedumu kwenye madaraka milele. Hakuna anayekuwa tajiri milele. Hakuna anayekuwa maskini milele. Vyote hivi ni vya muda tu. Ni suala la majira na nyakati

*Mtu unayemdhihaki leo na kumuona sawa na takataka, inawezekana ndiye atakayeamua hatma ya maisha yako kesho*. Mheshimu kila mtu bila kujalisha yupo katika hali gani leo kwa sababu huwezi jua kesho atakuwa wapi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad