Vanessa Mdee Afunguka Kinachomuogopesha Kuingia Kwenye Ndoa

Vanessa Mdee Afunguka Kinachomuogopesha Kuingia Kwenye Ndoa
LICHA ya kwamba yupo kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa muda mrefu na mwanamuziki mwenzake, Juma Jux, mwanadada Vanessa Mdee ‘Vee Money’ ametaja sababu zinazomuogopesha kuingia kwenye ndoa.



Akichonga na Mikito Nusunusu, Vee Money alisema licha ya kwamba ana umri wa miaka 30 kwa sasa, lakini hajawaza kuolewa kwa sababu anaogopa atabanwa na majukumu ya ndoa na kushindwa kufikia malengo aliyonayo.



“Umri wangu umefikia wa kuingia kwenye ndoa, lakini siwezi kwani nina malengo makubwa ambayo bado sijayatimiza hadi sasa hivyo nahofia nikiingia kwenye ndoa kuwa nitabanwa na kushindwa kuyatimiza, maisha ni malengo hivyo siwezi kukurupuka tu, nikishayatimiza hayo malengo ndipo nitaingia kwenye ndoa,” alisema Vee Money.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad