Vyama Pinzani vyamcharukia Jaji Mutungi, kuahirisha kikao

Vyama Pinzani vyamcharukia Jaji Mutungi, kuahirisha kikao
Naibu katibu mkuu wa Chadema (Zanzibar), Salum Mwalimu amefunguka na kusema kuwa wamestushwa na ahirisho la ghafla la msajili wa vyama vya siasa Jaji Francis Mutungi akiwaeleza watanza nia na vyama vya siasa kwamba ameahirisha kikao cha baraza cha tarehe 21 na 22 kilichokua kifanyike Zanzibar.

Salum Mwalimu ameyasema hayo leo Dec 22, 2018 katika kikao cha viongozi wakuu wa vyama vya upinzani, ameongeza zaidi kuwa Jaji Francis Mutungi hana mamlaka ya kuahirisha kikao hicho kwa sababu yeye ni katibu.

Akienda mbali zaidi Salum Mwalimu amesema, Jaji Mutungi kwenye taarifa yake kwa umma na vyama vya siasa ametaja kwamba ameshirikisha na kushauriana na kamati ya uongozi hivyo basi amemtaka awataje hao watu alioshirikiana nao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad