Wabunge nchini Somalia wamewasilisha hoja bungeni ya kutaka kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais Mohammed Abdullahi Farmajo.
Mmoja wa wabunge ambaye amechochea hoja hiyo Abdifitah Ismail Dahir ameiambia BBC wanamtuhumu Rais kwa uhaini baada ya kusaini makubaliano ya kisiasa na kiuchumi na Ethiopia na Eritrea.
Amesema Rais ameshindwa kuwashirikisha taarifa wenzie kuhusiana na makubaliano yanayohusisha bandari za Somalia.
Wanamlaumu pia Rais kwa madai ya kuwarejesha wahalifu isivyo halali.
Wabunge wapatao 92 wanapaswa kusaini hoja hiyo ya kutokuwa na imani na Rais, kuweza kuwasilisha kwa Spika, ili aruhusu kuanza kwa mjadala.
Mizozo ya kisiasa ni jambo la kawaida nchini Somalia na utata huo wa hivi karibuni umekuja wakati serikali ikikosolewa kwa kuingilia kati uchaguzi wa majimbo.
Wabunge wa Somalia Waandaa Hoja ya Kutokuwa na Imani na Rais
0
December 10, 2018
Tags