Wachimbaji wadogo zaidi ya elfu 10 wavamia mashamba ya kijiji


Wachimbaji wa dhahabu wadogo zaidi ya elfu kumi, kutoka mikoa ya Geita, Shinyanga na Simiyu wamevamia katika mashamba ya Kijiji cha Bulumbaka Kata ya Mwaobingi, Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Vijijini, kwa madai ya kuwepo kwa madini ya dhahabu katika Kijiji hicho, wakiiomba Serikali kupeleka wataalam wa madini haraka ili waweze kuchimba kwa uhakika.

Aidha umati mkubwa wachimbaji wadogo wa dhahabu wakiwa na dhana zao, ambapo inadaiwa kuwa uvumi wa kuwepo kwa madini katika kijiji hicho ulianza siku mbili zilizopina na kusababisha wachimabi kutoka mikoa ya Shinyanga na Geita kuwasilia mkoani Simiyu kwa ajili ya uchimbaji.

Akizungumzia kuhusu uwepo wa madini katika eneo hilo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Vijijini James John anasema kwa sasa wamewataka wachimbaji hao kuwa na subira ili kuhakikisha kama kweli kuna madini na kwamba wataalamu wa madini wanaendelea na uchunguzi wao

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad