Wagombea wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Condo wamelalamikia dosari nyingi wanazosema zilitokea wakati wa uchaguzi wa urais uliofanyika Jumapili.
Milolongo mirefu ya wapiga kura ilishuhudiwa katika vituo vingi na mitambo ikafeli kwenye baadhi ya vituo.
Aidha, upigaji kura uliathiriwa katika baadhi ya maeneo baada ya mvua kubwa kunyesha, huku baadhi ya wapiga kura wakilalamikia majina yao kutokuwepo kwenye sajili katika baadhi ya vituo.
Mmoja wa wagombea wa urais wanaotaka kumrithi Rais Joseph Kabila anayeondoka baada ya kuongoza kwa miaka 17, Felix Tshisekedi, amesema anahofia kwamba huenda hitilafu hizo zilipangwa ndipo kutoa sababu za uchaguzi kufutwa na kumuwezesha Bw Kabila kusalia madarakani.
Wengi wa wapiga kura walitatizika kutokana na hali kwamba mashine zilitumiwa kwa mara ya kwanza kupigia kura.
Aidha, baadhi ya mashine zilifeli.
Shughuli ya kuhesabu kura zilizopigwa inaendelea baada ya vituo kufungwa Jumapili jioni na matokeo rasmi yanatarajiwa kutangazwa katika kipindi cha wiki moja.
Uchaguzi wa sasa ulifaa kufanyika miaka miwili iliyopita lakini uliahirishwa mara kadha kutokana na kutokamilika kwa maandalizi.
Kabla ya uchaguzi, kulitokea utata baada ya uchaguzi kuahirishwa katika maeneo yaliyoathiriwa na Ebola yakiwemo miji ya Beni na Butembo mashariki mwa nchi hiyo, na pia katika jiji la Yumbi magharibi mwa nchi hiyo.
Hatua hiyo iliathiri takriban wapiga kura 1.26 milioni kati ya jumla ya wapiga kura 40 milioni. Uchaguzi katika maeneo hayo uliahirishwa hadi Machi.
Uamuzi huo ulizua utata ikizingatiwa kwamba rais mpya anafaa kuapishwa kufikia katikati mwa Januari.
Baadhi ya wanaharakati waliandaa uchaguzi wa mwisho uliopewa jina 'uchaguzi wa raia' katika mji wa Goma, mojawapo wa miji iliyoathiriwa, anasema mwandishi wa BBC Gaius Kowene
Wagombea was Upinzani Walalamikia Dosari za Uchaguzi wa Urais DRC
0
December 31, 2018
Tags