Baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wamesema wanamsubiri kwa hamu Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu apitishwe na chama chake kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2020.
Lissu anayetibiwa nchini Ubelgiji baada ya shambulio la risasi zaidi ya 30 lililotokea Septemba 7, mwaka jana akiwa Dodoma, juzi aliliambia gazeti la Mwananchi kwamba hatakuwa na kipingamizi ikiwa chama chake kitampitisha kuwania nafasi hiyo.
Kauli ya Lissu ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa Serikali ya CCM, imepokewa kwa furaha na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wakiamini anaweza kutoa ushindani mkubwa kwa mgombea wa chama tawala.
Mwenyekiti wa Chaumma, Hashim Rungwe alisema Lissu atavifaa vyama hivyo katika Uchaguzi Mkuu wa 2020.
Maoni ya Rungwe yaliungwa mkono na Kiongozi wa ACT – Wazalendo, Zitto Kabwe ambaye alisema hana shida na kauli ya Lissu.
“Jambo la muhimu kuliko yote ni kuwa mwaka 2019, kwetu ni mwaka wa kudai demokrasia. Azimio la Zanzibar limeweka mpango maalumu wa kukabiliana na ukandamizaji wa demokrasia. Tundu Lissu ni kiongozi muhimu katika harakati hizo,” alisema Zitto.
Pia, Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye alisema Lissu hajafanya kosa kutoa kauli hiyo kwa sababu mwanachama yeyote anaweza kueleza nia yake.
“Sijamsikia, lakini kama atapitishwa na chama sioni tatizo, kwa sababu kila chama kina utaratibu wake wa kuwapata wagombea na ni lazima ufuatwe,” alisema Sumaye.
Sumaye ambaye ni mjumbe wa kamati kuu ya Chadema mwenyekiti wa Kanda ya Pwani wa chama hicho alisema Lissu si wa kwanza, “Nimemsikia hata mheshimiwa (Edward) Lowassa, mimi sioni tatizo kama mtu anafuata utaratibu wa chama.”
Walichokisema Sumaye, Zitto Kabwe Baada ya Tundu Lissu Kusema Yupo Tayari Kugombea Urais 2020
2
December 28, 2018
Tags
Mhhh....!!!!
ReplyDeleteHivyo mmetuona sisi nni mazuzu Watanzania!!!!
Mnajifurahisha na Saccos ya Mtowe ..Kama ni Ruzuku hatakugawieni basi kamuulizeni Mh Mwita atakupeni mchogo alio ustukia...!!!
Nchi yetu haitaki Magoi goi na Viwete
Tunataka Jembe chapa ya Nyati aau Faru.
Sasa nikupeni SIRI,,,!!!!?
Jembe hilo lipo tayari
Baba laoooo!!!!
Niseme Nisise?????????
Bibi na Babu waliniambia hilo Jembe limetoka kwa kina Ngoossha h7k mbali
Chatoooooo.
SI MWINGINE ILA NI MJUKUU WETU
KI MAGU CHETU. MUNGU AMLINDE NA AMPE AFYA NA UMURI TAWILI AENDELEE KUTUTUMIKIA JINA LAKE NI ..JPJM
ZZIBA HEWA MASH7HUI DUNIANA NA MKEREKETWA WA UFISADI NA UBADHIRFU WA MALI ZA NCHI YETU NA NI MLETA MAENDELEO BILA UBAGUZI.
CHA ZAIDI NI MZALENDO ASIYE KIFANI..!
ukitaka kujuaMuulize hata Narenda Modi na Abdul Atah al Sisi siyo Siri anakubalika Uiimwenguni kote.
Lizzu wewe uje uendelee na mama Cheza hapa Moi. tunakuahidi kitanda utapata huwezi kulazwa chini.
Siasa waachie wana Siasa kama alivyo ibu babaZero hapo juu. HUna Chako..!!
Pole tena sana.....!!!!
Ni kama hujielewi vile naiona akili ndogo sana inayoishi kwa mihemko ya kijuha. Hivi unaanzaje kuulizia ruzuku ya chama kingine wakati huijui ruzuku ya chama chako? Kwanini usiulize kwanza matumizi ya ruzuku ya chama chako? Watz wenye akili timamu unawaeleza habari za Mwita? Are you stupid may be? Njoo na mapato na matumizi ya chama chako halafu ndipo uanze kusema uongo wako, otherwise, you are fooling yourself.
Delete