Mbunge wa Jimbo la Tandahimba, Katani S Katani ameendelea kulalamikia utaratibu uliotumika na serikali katika kuwalipa wakulima wa korosho, ambapo amedai kuwa utaratibu huo una makosa.
Kwa mujibu wa Katani, serikali imekuwa ikitumia utaratibu wa kuwalipa wakulima wa zao hilo ambao wanaanzia idadi ya magunia 15, huku wenye idadi ya magunia zaidi ya 15 wakiwa hawajalipwa.
"Hakuna Mkulima mwenye gunia 16 amelipwa fedha za korosho kwenye jimbo langu mimi, wakulima hapa wanaweza kuvuna zaidi ya magunia 16. Kwa mwaka huu na mpaka sasa hawajalipwa fedha zao," amesema Katani.
Aidha Katani ameongeza, "mimi kwangu serikali imeshafanya uhakiki mkubwa lakini serikali, kuna baadhi ya hawajalipa na mpaka sasa imeshalipa bilioni 6 na hizo fedha ni sawa kukilipa chama kimoja wakati kwenye Jimbo langu kuna zaidi ya vyama 128."
Hivi Karibuni Waziri Japhet Hasunga amesema serikali mpaka sasa imeshalipa zaidi ya bilioni 133 kwa wakulima zaidi ya laki 130 katika mikoa ya Mtwara, Pwani, Lindi na Ruvuma.