Watanzania Wanapenda Sana Mapenzi Kuliko Kula- Queen Darleen

Watanzania Wanapenda Sana Mapenzi Kuliko Kula- Queen Darleen
Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB, Queen Darleen ameibuka na kuweka wazi sababu za kupendelea kuimba nyimbo za mapenzi.

Queen Darleen amesema anapenda sana kuimba nyimbo za mapenzi kwa sababu Watanzania wanapenda sana mapenzi kuliko kula kwaiyo nyimbo za mapenzi zimekuwa na soko zaidi Bongo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Queen Darleen ameweka wazi kuwa wasanii wengi Bongo soko lao lipo kwenye nyimbo za mapenzi ndio maana hata ukiangalia nyimbo hizo ndizo zinafanya vizuri zaidi.

Unajua Watanzania wanapenda sana Mapenzi kuliko kula kuliko hata kufanya kazi ndio maana nyimbo za mapenzi zinafanya vizuri zaidi kwenye Bongo fleva na ndio maana wakina Mbosso, Lavalva wanafanya vizuri na Diamond Mpaka leo yupo kwenye chati kisa nyimbo za mapenzi “.

Queen Darleen amesema anatamani Label ya WCB isaini Msanii wa kike ili yeye apate chagamoto ya kufanya kazi nzuri zaidi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad