Watanzania wanne waenda China kuiwakilisha nchi Katika Mashindano ya Dunia ya Kuogelea

 Watanzania wanne waenda China kuiwakilisha nchi
Waogeleaji wanne wameondoka nchini kuelekea nchini China, katika mashindano ya dunia ya kuogelea yatakayofanyika nchini China kuanzia Desemba 11 mpaka 16 huko 'Hangzhou Olympic and International Expo Center'.


Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Kuogelea nchini (TSA), Asmah Hilal amesema timu hiyo ya wanamichezo wanne imeondoka nchini usiku wa Disemba 7, na  imeambatana na kocha Alexander Mwaipasi na Mwenyekiti wa chama chao, Imani Dominick.

Waogeleaji ambao wamekwenda kwenye mashindano hayo ni Kalya Temba na Celina Itatiro kwa upande wa wanawake na Collins Saliboko na Hilal Hilal kwa upande wa wanaume.

Akiongelea maandalizi yao Asmah amesema, “Ni matarajio yetu kuwa watafanya vizuri pamoja na changamoto mbalimbali tunazokabiliana nazo, mashindano yatakuwa magumu kwani waogeleaji nyota wa Dunia nao watakuwepo''.

Mashindano haya ni ya 14 ambapo yatafanyika kwenye bwawa la kisasa la kuogelea lenye urefu wa mita 25. Pia Bwawa hilo linahamishika na kwasasa lipo kwenye uwanja wa mchezo wa Tenisi lakini katika mashindano haya litaondolewa na kuwekwa eneo la wazi zaidi

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad