Ajali hiyo iliyotokea katika eneo la Ankara imehusisha treni ya mwendokasi iliyokuwa inaelekea katika ya mji wa Konya baada ya kugonga kiberenge kilichokuwa kinafanya uchunguzi
Ajali hiyo imetokea katika kituo cha treni Wilayani Yenimahalle baada ya treni ya mwendokasi kushindwa kumimama, hata hivyo uchunguzi zaidi unaendelea kujua chanzo cha treni hiyo kushindwa kusimama
Gavana wa Ankara, Vasip Sahin amesema utaratibu za uokoaji bado zinaendelea lakini bado haijafahamika treni hiyo ilikuwa ikisafiri kwa mwendokasi gani
Mwezi Julai, watu 10 walifariki na zaidi ya 70 kujeruhiwa baada ya treni ya abiria kutoka kwenye reli huko Kaskazini Magharibi mwa Uturuki
Mwezi uliopita, watu 15 walijeruhiwa baada ya treni ya abiria kugongana na treni ya mizigo katikati ya mji wa Sivas Konya, takribani Kilometa 260 Kusini Magharibi mwa Ankara