Watumia jina la waziri kutapeli


NAIBU Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Elias Kwandikwa, amesema limeibuka kundi la watu wanaotumia jina lake kuwatapeli wananchi kuwa atawatafuatia kazi ya udereva kwa makandarasi wanaoendelea na kazi mikoa mbalimbali nchini. 

Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu jana, Kwandikwa alisema watu hao wamekuwa wakiwatumia ujumbe wa maandishi kwa njia ya simu zao za mkononi na kuwaambia kuwa anahitaji kuwatafutia watu kazi ya udereva jambo ambalo si kweli. 

Alisema kikundi hicho kimekuwa kikitumia namba mbalimbali kuwatumia ujumbe wananchi katika simu za mkononi juu ya kuwatafutia kazi na kwamba wanafanya hivyo kutokana na yeye kuwa katika wizara yenye dhamana ya masuala ya ujenzi. 

“Ninafahamiana na makandarasi wengi wanaofanya kazi na nimezunguka nchi nzima kukagua miradi mbalimbali  ya ujenzi katika kazi zilizokamilika na zinazoendelea kutekelezeka. Sasa wanatumia mwanya huo kuwatapeli wananchi ili kujinufaisha,” alisema. 

Taarifa za watu hao kutumia jina lake kuwatapeli wananchi ameshazifikisha katika vyombo vya sheria, ili kuangalia namna ya kuwashugulikia na kuwataka wananchi kupuuza ujumbe huo kwa kuwa si kweli kwamba anahitaji kuwatafutia watu ajira kwa makandarasi.  

Pia alisema kama kuna mwananchi atapata ujumbe wowote kwenye simu yake juu ya kutafutiwa kazi, amtafute katibu wake wa jimbo kuhakikisha jambo hilo kama ni kweli au si kweli kwa kuwa kila jambo linalohusu jimbo, hivyo lazima katibu wake alifahamu.  

Aidha, Kwandikwa alizitaja namba simu ambazo zimekuwa zikitumika kwa ajili ya utapeli huo kuwa ni 0653 503578 na 0655 146152.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad