Wayne Rooney: Mourinho Alichukiwa Hadi na Wadada wa Jikoni’

Aliyekuwa mchezaji wa Manchester United, Wayne Rooney amesema anaamini kuwa wafanyakazi wengi wa timu hiyo hawakuwa na furaha na Jose Mourinho.


Mreno huyo alitimuliwa kazi mapema wiki hii baada ya kuwa namwanzo mbaya wa msimu huku akiwaacha United kwenye nafasu ya sita msimamo waligi kuu Uingereza na hatua ya 16 bora michuano ya Champions League.

Mourinho was removed from his position this week following a torrid start to the season
Rooney anaamini kocha mpya wa timu hiyo, Solskjaer ndiye mtu sahihi atakayeweza kubadilisha upepo mbaya wa Old Trafford huku akiiyambia BT Sport kuwa si kwa wachezaji pekee bali kwa klabu nzima.

Ole Gunnar Solskjaer has replaced him and takes charge of his first game on Saturday night
‘’Nina hakika Ed Woodward alikuwa sawa tu nawengine, wafanyakazi wote, madada ambao ni wapishi wajikoni, watunza vifaa wote hawakuwa na furaha naye. Ole ndiye mtu pekee atakayeweza ipeleka timu hii kwenye mstari uliyonyooka  na nafahamu wote sasa wanafuraha,’’ amesema Rooney.

Ole Gunnar Solskjaer amechaguliwa kurithi nafasi ya Mourinho kwa muda na kwa mara ya kwanza amekiongoza kikosi cha United kwenye ushindi wa mabao 5 – 1 dhidi ya Cardiff.

Paul Pogba looked happy as he arrived at the Cardiff City Stadium for Saturday's match
Wayne Rooney ambaye anaangaziwa kama legendi Old Trafford ameongeza ‘’Ili kufanikiwa kwenye soka unahitaji kila kitu kuwa sawa, mahusiano yako na wafanyakazi wenzako pamoja na wachezaji lakini hali ilikuwa tofauti.’’

‘’Kwa sasa wachezaji wameanza kurejea tena na nimwendo mzuri kwa klabu, niwakati wa kumuangalia, Ole anavyopanga timu yake na namna wanavyocheza.’’

Rooney anaamini ni wakati muhimu sasa kuwarudisha wachezaji kuwa wamoja ili kufurahia soka na kumfanya kocha, Solskjaer kukirejesha kikosi hiko kwenye makali yake.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad