Waziri 'ajivunia' kukamata madiwani 11 CCM


Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina amekiri kukamatwa kwa madiwani 11 wa Chama Cha Mapinduzi CCM kwa tuhuma za uvuvi haramu katika halmashauri ya CHATO mkoani Geita.


Akizungumzia tukio hilo, Waziri Luhaga Mpina amedai viongozi hao wamekiri kosa na wameomba msamaha huku akiangalia utaratibu wa kuwalipisha faini au kuwapeleka mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

"Wako madiwani tena wa CCM, na Mwenyekiti wa hamashauri Chato ambaye nayeye ni kutoka CCM,  wameshiriki kwenye uvuvi haramu niwaambie tu wamekuja na hakuna aliyebisha na wote wameendelea kuomba msamaha japo sijawapa majibu tutaamua nini," amesema.

"Tunaweza kuamua kufuta adhabu ya faini ili tuwashtaki tuwafikishe mahakamani, sababu huwezi ukawa diwani wa wananchi umekabidhiwa mamlaka kulinda rasilimali lakini ajabu wewe ndiyo unaongoza uhalifu."

"Maamuzi yangu mengine nitakayo fanya ni kuwanyang'anya kukusanya mapato, ili zirudi serikalini, haiwezekani Mkurugenzi wa pale mwenyekiti wake anashiriki uvuvi haramu halafu yeye hajui," ameongeza Luhaga Mpina.

Mapema wiki hii Waziri Mpina alibainisha serikali kutomvumilia mwananchi yeyote ambaye atathibitika kukiuka sheria na taratibu za uvuvi zilizowekwa na serikali lakini kwa wale ambao watakamatwa nje ya nchi serikali haitahusika kwa lolote juu yake.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad