Waziri Mkuu Aingilia Kati Mgogoro wa Mkuu wa Mkoa na Wakuu wa Wilaya Kilimanjaro Awatuma Mawaziri Wawili Kwenda Kutatua Tatizo

Waziri Mkuu  Aingilia Kati Mgogoro wa Mkuu wa Mkoa na Wakuu wa Wilaya Kilimanjaro Awatuma Mawaziri Wawili Kwenda Kutatua Tatizo
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewaagiza mawaziri wawili katika Ofisi ya Rais kwenda mkoani Kilimanjaro kutatua tatizo la uhusiano kati ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira na wakuu wa wilaya za mkoa huo.

Mawaziri waliopewa maagizo hayo wakati Majaliwa akifungua mafunzo ya wakuu wa mikoa na makatibu tawala wa mikoa ya Tanzania Bara leo Jumatatu Desemba 3,  2018 ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi), Seleman Jafo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora),  George Mkuchika.

Majaliwa amesema wakati mwingine kauli na hatua ambazo si muhimu zinaweza kuifanya Serikali kuonekana  si sekta muhimu.

“Mheshimiwa waziri ameeleza hapa juu ya matumizi ya adhabu ya kuweka watu ndani. Tumeona mabishano haya kati ya kiongozi wa mkoa na wakuu wa wilaya wanapochukua hatua lakini bado kuna shida,” amesema Majaliwa.

“Nataka niagize waziri wa Tamisemi nenda mkoani Kilimanjaro bado kuna shida. Kuna shida ya mahusiano kati ya mkuu wa mkoa na wakuu wa wilaya tena wengi sio mmoja.”

Amemuagiza pia Mkuchika atakapopata muda kwenda Kilimanjaro aendeshe semina ya wakuu wa wilaya juu ya itifaki na kuheshimu mamlaka ya watu wengine ili kuwezesha mkoa kufanya kazi yake vizuri.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad