Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu Afunguliwe Mashtaka ya Ufisadi - polisi

Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu Afunguliwe Mashtaka ya Ufisadi - polisi
Polisi nchini Israel wamependekeza kufunguliwa mashtaka waziri mkuu Benjamin Netanyahu na mke wake Sara kwa madai ulaghai na ufisadi.

Wanashukiwa kuipendelea kampuni ya mawasiliano ya Bezeq telecom ili nayo iweze kuwapendelea kwa kuandika taarifa nzuri kuwahusu.

Bw Netanuyahu alikana madai hayo yanayojulikana kama Case 4000.

Mwanasheria mkuu nchini Israel sasa ataamua ikiwa ataleta mashtaka kuhusu madai hayo.

Kwenye taarifa ya leo Jumapili Bw Netanyau alisema: "Mapendezo haya yalifuja hata kabla ya uchunguzi kuanza.

"Nina uhakika kuwa katika kesi hii, mamlaka zinazoangalia suala hili zitafikia uamuzi ule ule kuwa hakuna chochote kwa sababu hakuna."

Ndege hatari zaidi ya kivita duniani yatumiwa na Israel
Trump: Jerusalem ni mji mkuu wa Israel
Waziri wa Ulinzi ajiuzulu Israel
Netanyahu aishambulia Iran akiita "chui milia hatari"
Mwezi Februari polisi walipendekeza kufunguliwa mashtaka Bw Netanyahu katika kesi zingine mbili za ufisadi.

Ametupilia mbali madai yote kuwa yasiyo na msingi.

Vyombo vya habari nchini Israel vinasema kuwa wachunguzi wamemhoji Netanyahu mara kadhaa.

Netanyahu, 69, anaongoza muungano tete lakini anaamini kuwa madai hayo hayawezi kuchochea uchaguzi wa mapema.

Uchaguzi wa bunge unapangwa kufanyika Novemba 19. Bw Netanyahu anahudumu awamu yya pili kama waziri mkuu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad