Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga amesema namna ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli anavyoongea na kutenda ni sawa na Mwasisi wa Taifa la Tanzania, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Hasunga ameyasema hayo alipotembelea eneo la Ihumwa ambapo ujenzi wa ofisi mpya za Wizara ya Kilimo zimeanzwa, Jijini Dodoma ambapo amesema Mwl. Nyerere ndiye aliyetoa wazo la Dodoma kuwa makao ya Chama Tawala pamoja na serikali lakini kwa miaka kadhaa wazo hilo lilikuwa halijawahi kutekelezwa na kuongeza kuwa Rais Magufuli ndiye amelitekeleza kwa vitendo.
“Napenda nimpongeze Mhe. Rais wetu kwa kulisimamia wazo hili la kuwa na eneo maalum na rasmi la kuwa ofisi kwa Wizara zote na moja kati ya faida ni kuwa Wananchi ambao wamekuwa wakisafiri kutoka mikoa mbalimbali kwa ajili ya kupata huduma katika ofisi za umma, sasa watapata unafuu wa kuhudumiwa katika eneo moja kama hapa, ambapo kila Wizara itapatikana", amesema Waziri Hasunga.
Waziri Hasunga ameongeza kuwa, jambo hili ni sawa na utekelezaji wa Oparesheni sogeza ambapo, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alianzisha katika mwaka 1974 lengo likiwa ni kuhakikisha Wananchi wanakaa pamoja ili Serikali iwahudumie kwa haraka zaidi na kwa ufanisi zaidi.
Waziri wa Kilimo Amfananisha Rais Magufuli na Nyerere
1
December 28, 2018
Tags
Hasunga mimi nitakusahihisha kidogo..!!
ReplyDeleteZama zetu na Mwalimu kulikuwapo na kulindana kwa kiasi Fulani.
akikupenda panga pangua wewe uko ndani
sana sana atakubadilisha Wizara au anapaa Wdhifa Mwigine. Lakini ni upo tu na ulaji unaendelea nao.
Na hii iikuwa na sababu na ulipaji wa wadhila na changamoto za wakati.
Lakkini Magu wetu ni PERFOMANCE DRIVEN
HA AGALI SURA WALA KUMUONEA HAYA MTU AU UKARIBU WAKE AU UHUSIANO WA UNDUGU NA URAFIKI WA UKARIBU.
MAGU IS FAIR PLAYER AND MAKES decision 8 timely manner.
HE IS extraordinary .
TOMY OPINION HE IS THE BEST OF OUR TIME.
MUNGU AMLAZE MAHALI PEMA MWALIMU.